Na Saulo Stephen - Singida.
Katika kuboresha huduma ya Afya na kuwa na uhakika wa matibabu kwa wagonjwa hususani akina Mama na Watoto, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovic, amepokea vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya huduma za akina mama na watoto katika Hospitali ya Manispaa ya Singida.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Dkt. Victorina amesema sekta ya afya mkoani humo imeendelea kuimarika kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali, ikiwemo ujenzi wa hospitali mpya, kuongezeka kwa watumishi wa afya pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa. Ameongeza kuwa vifaa vilivyopokelewa vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya, hususan kwa mama na mtoto, kwa kuongeza ufanisi na kasi ya huduma zinazotolewa katika vituo vya afya.

Ameongeza kuwa ujio wa vifaa hivyo ni fursa muhimu kwa wananchi, hususan wanawake, kupata huduma bora na salama za afya ya uzazi na watoto, huku akihimiza wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha sekta ya afya.
Miongoni mwa Vifaa hivyo ni pamoja na mashine za kufuatilia mapigo ya moyo wa mtoto (fetal dopplers), vifaa vya uangalizi wa watoto wachanga (neonatal resuscitation equipment), pamoja na mashine za kupima shinikizo la damu na kiwango cha damu kwa wajawazito.



Discussion
Reader comments
0 contributions