Skip to main content

DKT. LEBBA, VIONGOZI WA DINI ITIGI WAJADILI MASUALA YA LISHE BORA KATIKA JAMII

Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali katika Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, wamepatiwa mafunzo ya lishe bora kwa lengo la kutambua umuhimu wa lishe katika jamii.

DKT. LEBBA, VIONGOZI WA DINI ITIGI WAJADILI MASUALA YA LISHE BORA KATIKA JAMII
Studio Narration JAMBO FM

DKT. LEBBA, VIONGOZI WA DINI ITIGI WAJADILI MASUALA YA LISHE...

0:00 --:--

Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali katika Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, wamepatiwa mafunzo ya lishe bora kwa lengo la kutambua umuhimu wa lishe katika jamii.

Kikao hicho kimefunguliwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba, ambapo amesema kupitia uongozi wake ameweka msisitizo katika ushirikiano kati ya wataalamu wa afya na viongozi wa dini ili kuhakikisha elimu sahihi kuhusu lishe bora inawafikia wananchi wengi zaidi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba

Mafunzo hayo ni sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya maamuzi sahihi kuhusu ulaji, kupunguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta kwa wingi, na kuzingatia vyakula vya asili kwa ajili ya kulinda afya na kuboresha ustawi wa maisha.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Dini pamoja na wataalamu wa Afya ,Itigi Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.