Skip to main content

DKT. DUGANGE ATAJA SILAHA UTOKOMEZAJI NDOA ZA UTOTONI

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu, malezi bora na ulinzi wa mtoto wa kike ili kutokomeza ndoa za utotoni nchini.

DKT. DUGANGE ATAJA SILAHA UTOKOMEZAJI NDOA ZA UTOTONI
Studio Narration JAMBO FM

DKT. DUGANGE ATAJA SILAHA UTOKOMEZAJI NDOA ZA UTOTONI

0:00 --:--

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu, malezi bora na ulinzi wa mtoto wa kike ili kutokomeza ndoa za utotoni nchini.

Amesema mtoto wa kike anapaswa kupewa fursa ya kukua, kupata elimu na kujiandaa kikamilifu kabla ya kuingia katika ndoa, akieleza kuwa ndoa za utotoni zina athari kwa afya, elimu na ustawi wa familia.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika Oktoba 20, 2026 Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga, yenye kaulimbiu “Tokomeza Ndoa za Utotoni, Wekeza katika Haki za Wasichana,”

Dkt. Dugange amesema ujauzito katika umri mdogo huongeza hatari za kiafya kwa mtoto wa kike na mtoto anayezaliwa, huku ukosefu wa elimu na fursa za kiuchumi ukisababisha umaskini katika familia.

Aidha, Dkt. Dugange amesisitiza kuwa juhudi za kumlinda na kumwezesha mtoto wa kike zinapaswa kwenda sambamba na elimu na malezi kwa mtoto wa kiume.

Ameeleza kuwa wazazi na jamii wana jukumu la kuwajenga watoto wa jinsia zote katika misingi ya uwajibikaji, heshima na kupinga ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amewahimiza vijana kujiamini, kuendeleza vipaji vyao na kushiriki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Ameeleza kuwa Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau kuweka mazingira salama kwa vijana, huku akibainisha changamoto za ukatili zinazowakabili watoto wa kiume, ikiwemo ulawiti.

Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha watoto wa kike na wa kiume wanapata haki sawa katika elimu, huduma za afya na fursa za kujenga maisha bora.

Dkt. Dugange pia ametambua nafasi ya Femina Hip kupitia vilabu vya Fema, ambavyo kwa zaidi ya miongo miwili vimekuwa vikitoa fursa kwa vijana kujenga uongozi, kujiamini na kushiriki majadiliano kuhusu changamoto zinazowahusu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.