Skip to main content

DKT. CHAYA KUWEKA KIPAUMBELE MIRADI YA MAENDELEO MANYONI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mkoani Singida, Dkt. Pius Chaya amesema, ataweka kipaumbele katika miradi ya elimu, afya, barabara na masoko katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha maendeleo ya wananchi wa jimbo la Manyoni.

DKT. CHAYA KUWEKA KIPAUMBELE MIRADI YA MAENDELEO MANYONI
Studio Narration JAMBO FM

DKT. CHAYA KUWEKA KIPAUMBELE MIRADI YA MAENDELEO MANYONI

0:00 --:--

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mkoani Singida, Dkt. Pius Chaya amesema, ataweka kipaumbele katika miradi ya elimu, afya, barabara na masoko katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha maendeleo ya wananchi wa jimbo la Manyoni.

Dkt. Chaya ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata ya Chikuyu, ambapo alikagua miradi ya maendeleo na kukutana na wananchi katika mikutano ya hadhara kwa lengo la kujadili mahitaji yao na kuweka msingi wa utekelezaji wa ahadi za maendeleo.

Katika ziara hiyo, alikagua maendeleo ya ujenzi wa darasa la elimu ya awali katika Kijiji cha Chilejeho, mradi unaolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na kuimarisha huduma za elimu katika eneo hilo.

Aidha akizungumza na wananchi, Dkt. Chaya aliwashukuru kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni na kueleza kuwa ziara hiyo inalenga kuwashukuru kwa imani waliyoonyesha kwake pamoja na kuweka bayana mipango ya maendeleo atakayofuatilia katika kipindi cha miaka mitano.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni,Mkoani Singida, Dkt. Pius Chaya,

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.