Skip to main content

DKT. CHAYA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANYONI, ATOA AHADI

Na Saulo Stephen - Singida.

DKT. CHAYA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANYONI, ATOA AHADI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mkoani Singida, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Sasilo, Heka na Chikola, huku akiahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa vipaumbele vya wananchi.

Katika ziara hiyo, Dkt. Chaya alitembelea Jengo la Kujifungulia Wazazi katika Kituo cha Afya Sasilo, akakagua madarasa matatu ya Shule ya Msingi Chidamsulu pamoja na mradi wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Kizigo ili kujionea hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.

Mbali na ukaguzi wa miradi, Dkt. Chaya alizungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara‎“Tutatekeleza vipaumbele vya wananchi wa kila kata baada ya kutuamini tena,” alisema Dkt Chaya

Ameongeza kwa kusema kuwa, ataendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokusudiwa.

Wananchi na viongozi wa maeneo hayo walimpongeza Mbunge huyo kwa kufuatilia kwa karibu miradi ya maendeleo na kutumia mikutano ya hadhara kusikiliza mapendekezo yao, wakieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuharakisha maendeleo ya jimbo .

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.