Skip to main content

DKT. CHAYA: DIRA YA MAENDELEO 2050 KIPAUMBELE NI KUZALISHA AJIRA KUPITIA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI

Na Saulo Stephen - Singida.

DKT. CHAYA: DIRA YA MAENDELEO 2050 KIPAUMBELE NI KUZALISHA AJIRA KUPITIA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI

Na Saulo Stephen - Singida.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeweka mkazo katika kuongeza fursa za ajira kwa kushirikisha Serikali na sekta binafsi ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.

Dkt. Chaya, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Sanza, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Amesema chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Serikali inatarajiwa kuchangia takribani asilimia 30 ya ajira, huku sekta binafsi na wawekezaji wakibeba jukumu la kuzalisha asilimia 70 ya ajira zote nchini.

"Ajira ni suala la mtambuka ambalo haliwezi kubebwa na Serikali pekee. Ndiyo maana tunasisitiza ushirikiano mkubwa na sekta binafsi ili kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania," amesema Dkt. Chaya.

Amefafanua kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi, huku akisisitiza kuwa kila mwekezaji anayekuja nchini anapaswa kueleza wazi idadi ya ajira atakazozalisha kupitia mradi wake.

Kwa mujibu wa Dkt. Chaya, hatua hiyo itasaidia kuhakikisha uwekezaji unaofanyika nchini unaleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi kupitia ajira, ukuaji wa uchumi na kuimarisha maisha ya Watanzania.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akieleza kuwa ushiriki wa sekta binafsi ni nguzo muhimu ya kufikia maendeleo endelevu na kuongeza ustawi wa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.