Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani ya nchi na kushirikiana na Serikali, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, ambapo amezindua madarasa matano, matundu sita ya vyoo pamoja na Ofisi ya Walimu katika Shule ya Msingi Jitirola, kabla ya kutembelea na kukagua Zahanati ya Kiriba na kuzungumza na wananchi.

Amesema, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya elimu nchini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya shule pamoja na kuongeza walimu, ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora na kufikia malengo yao.
Katika hatua nyingine, Dkt. Bashiru amewapongeza wananchi kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa nguvu kazi na michango katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwataka kuendelea kuwahimiza watoto kupata elimu na kusimamia maendeleo yao.

Akizungumza na wananchi wa Kiriba, Dkt. Bashiru amewataka kulinda amani na utulivu uliopo nchini, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo.
Amesema, Serikali itaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii, ikiwemo elimu na afya, na kwamba ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ni muhimu katika kufanikisha maendeleo.

Aidha, Dkt. Bashiru pia mewataka wananchi kutunza miundombinu inayojengwa, kudumisha amani na kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.



Discussion
Reader comments
0 contributions