Skip to main content

DIWANI AONGOZA WANANCHI UJENZI WA ZAHANATI

Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Jackline Isaro, amewaongoza wananchi wa kata hiyo katika zoezi la uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Zahanati itakayohudumia zaidi ya wakazi 2,000 utakao gharimu kiasi cha shilingi Milioni 128 unaotarajiwa kukamilika mwaka 2027.

DIWANI AONGOZA WANANCHI UJENZI WA ZAHANATI
Studio Narration JAMBO FM

DIWANI AONGOZA WANANCHI UJENZI WA ZAHANATI

0:00 --:--

Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Jackline Isaro, amewaongoza wananchi wa kata hiyo katika zoezi la uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Zahanati itakayohudumia zaidi ya wakazi 2,000 utakao gharimu kiasi cha shilingi Milioni 128 unaotarajiwa kukamilika mwaka 2027.

Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Jackline Isaro akishiriki uchimbaji wa msingi wa Zahanati

Amesema uongozi wa Serikali ya Kata hiyo, kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa unaendelea kutatua changamoto za wananchi katika Kata hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na ahadi zake alizozitoa wakati akinadi sera zake kwa wananchi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Kinachoendelea kwa sasa ni kwa mujibu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na ahadi zangu nilizozitoa kwa wananchi wa kata hii. Niwaahidi kuwa Serikali hii itaendelea kutatua changamoto awamu kwa awamu,” amesema .

Baadhi ya wakazi Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakishiriki uchimbaji wa msingi wa Zahanati

Mbali na hilo amesema uongozi wa kata hiyo unaendelea na jitihada za kukabiliana na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha mwanzoni mwa mwezi Oktoba, huku akiwasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kukabiliana na janga hilo.

“Sisi kama viongozi, jukumu letu ni kusimamia hatua za kukabiliana na mvua hizi, japo tunawakumbusha wananchi wetu kuendelea kuweka mazingira rafiki katika makazi yao,” amesema Mh.Isaro.

Baadhi ya wakazi Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakishiriki uchimbaji wa msingi wa Zahanati

Nao baadhi ya wananchi kutoka kata hiyo waliojitokeza katika zoezi la uchimbaji wa msingi wa zahanati hiyo, akiwemo Jackson Masingija na Zera Sengimluka, wameipongeza hatua hiyo iliyofikiwa na Serikali ya kusogeza huduma za afya karibu hali itakayowaondolea adha ya kufuata huduma za matibabu nje ya kata hiyo.

"Tunaishukuru serikali yetu kwa kutazama changamoto tunazokutana nazo katika kupata huduma za afya. Awali tulikuwa tunapata tabu, hasa mgonjwa anapohitaji huduma ya haraka,” walisema wananchi hao.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Kata ya Ngokolo ina jumla ya wakazi 25,000, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.