Skip to main content

DIRA YA TAIFA 2050: MABORESHO YA SHERIA YAMEANZA KULINGANA NA MAHITAJI - HOMERA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

DIRA YA TAIFA 2050: MABORESHO YA SHERIA YAMEANZA KULINGANA NA MAHITAJI  - HOMERA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera amesema Serikali Nchini, imeanza maboresho ya sheria mbalimbali ili kuendana na mahitaji ya maendeleo ya muda mrefu pamoja na kuondoa Sheria zitakazo kuwa kikwazo katika utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050.

Waziri Dkt Homera ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Machi 23,2026 wakati akifungua Kikao cha nne cha Baraza la nane la wafanyakazi wa wizara hiyo ambapo amesema hakuna Sheria itakayo vumiliwa kama inakwamisha utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050.

Amesema kupitia baraza hilo watumishi wapaswa kupanga bajeti pamoja na ustawi wa taasisi bila kusahau kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kwenda sambamba na dira hiyo.

Pia amesema kufikiwa kwa Dira ya 2050 kunategemea uwepo wa sheria imara lakini pia rafiki kwa maendeleo, akionya kuwa bila maboresho hayo, malengo ya taifa yanaweza kuchelewa kufikiwa.

Hivyo, ameutaka mkutano huo kuhakikisha bajeti ya mwaka 2026/27 inaweka mkazo katika kuimarisha mfumo wa sheria na taasisi zake.

‎Katika kikao hicho, wajumbe wamejadili pia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/26, wakitathmini mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza. Lengo ni kuhakikisha rasilimali zinazotolewa zinatumika kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

‎Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, amesema majadiliano hayo yanaenda mbali zaidi ya bajeti, kwani ni mchango wa moja kwa moja katika kufanikisha dira ya taifa huku akieleza kuwa wizara imejipanga kuhakikisha sekta ya sheria inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi.

‎Naye, Mwakilishi wa TUGHE Mkoa Samwel Ngungwa amesema watahakikisha maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wanayafanyia kazi. 

‎Kwa mwaka wa fedha 2026/27, wizara inatarajia kuimarisha utawala wa sheria, kuongeza upatikanaji wa haki kwa wakati na kupanua matumizi ya teknolojia katika huduma za kisheria.

Hatua hizi zinatarajiwa kusaidia kuondoa urasimu na kuongeza ufanisi, huku zikiweka mazingira rafiki kwa maendeleo ya taifa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.