Skip to main content

DILI LA ULOZI: WACHAWI WALIVYONUFAIKA NA 'PROJECT STARGATE' YA MAREKANI

Ulikuwa ni mpango mkakati ukifahamika kama "Project Stargate" wa Marekani, na hiki ndicho chanzo cha uvumi wote wa "Marekani inasaka mchawi" ukiwa ni mpango wa kweli kwa 100% na CIA wenyewe ilithibitisha.

DILI LA ULOZI: WACHAWI WALIVYONUFAIKA NA 'PROJECT STARGATE' YA MAREKANI
Studio Narration JAMBO FM

DILI LA ULOZI: WACHAWI WALIVYONUFAIKA NA 'PROJECT STARGATE'...

0:00 --:--

Ulikuwa ni mpango mkakati ukifahamika kama "Project Stargate" wa Marekani, na hiki ndicho chanzo cha uvumi wote wa "Marekani inasaka mchawi" ukiwa ni mpango wa kweli kwa 100% na CIA wenyewe ilithibitisha.

KILICHOTOKEA MAREKANI (1972 - 1995).

Wakati wa Vita Baridi (Cold War), Marekani ilisikia kuwa Urusi inaajiri wachawi, waganga na watu wenye uwezo wa kuona mbali kwa akili (psychics) ili kuiba siri za kijeshi za Marekani.

CIA ikaogopa ikasema: "Kama Urusi ina wachawi, na sisi lazima tuwe na wachawi wetu!", hivyo wakaunda mipango ya siri wakiipa majina ya:

-GONDOLA WISH

- GRILL FLAME

- CENTER LANE

-SUN STREAK

- STARGATE

Waliajiri watu takriban 20-30 walioitwa "Remote Viewers" - kwa lugha ya kawaida ni wachawi wa kisasa.

Kazi zao:

1. Kumtafuta Gaddafi wa Libya mwaka 1986 kabla ya Marekani kumpiga bomu.

2. Kutafuta meli ya nyuklia ya Urusi iliyopotea baharini mwaka 1979.

3. Kutafuta ndege iliyoanguka ya Urusi* msituni Zaire (Congo sasa) - na hapa ndipo walipofanikiwa! Mchawi mmoja wa kike aitwaye Rosemary Smith alitaja coordinates, na ndege ikaonekana kweli baada ya siku 2.

4. Kutafuta mateka - Jenerali wa Marekani aliyetekwa na magaidi Italia.

5. Hata kuna faili moja la ajabu la 1984 ambapo mchawi aliambiwa aone Mars miaka milioni 1 iliyopita akasema aliona watu warefu, wembamba, wamevaa nguo za hariri, na piramidi kubwa!

Hapa ndipo lilipovuma neno WITCHES kwani Mwaka 1991, jeshi lilipoishiwa na wanaume wenye uwezo huo, waliajiri wanawake 2 wa kiraia:

- Angela Dellafiora

- Robin Dahlgren

Wanajeshi wa kiume waliwaita kwa dharau Wanawake hao "The Witches" (Wachawi) kwa sababu walikuwa wanatumia kadi za Tarot kusomea badala ya mbinu za kijeshi.

Mradi uligharimu dola Milioni 20 na ulifungwa rasmi 1995 baada ya CIA kusema matokeo yake yalikuwa 15% tu kwa eneo sahihi wakadai hayafai kutegemewa.

Kiuhalisia, Marekani haikutangaza ajira gazetini "Tunatafuta mchawi", lakini ndani kwa ndani CIA na Jeshi waliwaajiri wachawi/watabiri kwa siri kwa miaka 23 kutimiza majukumu ya kijasusi.

Andiko hili linathibitisha uvumi iliowahi kutanda siku za nyuma watu wakisema "Marekani inasaka mchawi", ni kweli ilisaka hapo zamani, si sasa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.