Skip to main content

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUTOA HUDUMA ZA AFYA KWA WELEDI, KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA, WATOTO - RC MHITA

Na Eunice Kanumba, Kishapu - Shinyanga.

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUTOA HUDUMA ZA AFYA KWA WELEDI, KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA, WATOTO - RC MHITA

Na Eunice Kanumba, Kishapu - Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amewapongeza wanawake wanaojifungua katika Hospitali ya Jakaya Kikwete iliyopo Wilayani Kishapu, akisema hatua hiyo inaonesha imani kubwa ya wananchi kwa huduma za afya zinazotolewa na Serikali kwani dhamira ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa weledi lakini pia kupunguza vifo kwa mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.

RC  Mhita ameyasema hayo Aprili 26, 2026 alipofika katika hospital hiyo    kwa lengo la  kutoa zawadi kwa wanawake waliojifungua katika Siku ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika kimkoa Wilayani Kishapu.

Amesema inatia faraja kuona wanawake wanatoa pongezi kwa Serikali kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya, hatua inayochochea ongezeko la kina mama kujifungulia katika vituo vya afya tofauti na siku na siku za nyuma na kwamba kufuatia utoaji wa huduma bora hizo za afya pamoja na kada zingine halimashuri ya wilaya ya Kishapu imeendelea kutengeneza mahusiano mazuri na makundi mbalimbali katika jimii  

“Ni jambo la kufurahisha kuona wananchi wanathamini jitihada za Serikali. Uwekezaji huu umeleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma za afya,” alisema RC  Mhita.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita  imeendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuongeza bajeti na kuboresha miundombinu pamoja na huduma, jambo linalogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, na kuwataka wahudumu wa afya kuendelea kutoa huduma na lugha nzuri kwa wagonjwa ili wananchi waendelee kufurahia huduma nzuri na sahihi wanazopewa na serikali yao.

Akizungumzia  muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika tarehe 26 APRIL 1964 chini ya viongozi wa waasisi wa mataifa hayo yaliyokuwa huru kipindi hicho, mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shekhe Abeid Amani Karume RC Mhita amesema muungano umeendelea kuleta mshikamano kati ya pande hizo mbili na kuwa alama sahihi ya Tanzania kufuatia kuimarika na kudumu kwa muda murefu na kuwa mfano wa kuigwa duniani.

Amewataka watanzania kuenzi na kujivunia  muungano uliopelekea kuzaliwa taifa la imara la  Tanzania na kuwaasa vijana kuendelea kulinda tunu hiyo iliyoachwa na waasisi wa taifa hili kwa kuendeleza amani na utulivu na upendo ili muungano huo uweze kudumu vizazi na vizazi vya taifa la Tanzania.

Kwa upande wao, baadhi ya wanawake waliopatiwa huduma ya kujifungua hospitalini hapo wamesema kwa sasa huduma zimeimarika kwa kiwango kikubwa, tofauti na ilivyokuwa hapo awali, na kuanisha kuwa wamepokelewa vizuri na kwa wakati na kusaidiwa ipasavyo kujifungua salama ambapo wameishukuru serikali kwa kuongeza majengo na vifaa tiba katika hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine katika  kusherehekea miaka 62 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari  wilaya ya Kishapu imepanda miti Zaidi ya milioni moja ili   kuendelea  kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na utunzaji wa mazingira ,  na kuhamasisha jamii iendelee kupanda miti inayostahimili ukame lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumzia suala hilo, RC Mhita ambaye naye ameshiriki zoezi hilo la kupanda miti amewataka wanchi wa kishapu kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika makazi yao kama inavyofanyika katika taasisi mbalimbali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.