Skip to main content

DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 110.05, CAG ATAKA USHAURI UFANYIWE KAZI

Hadi kufikia Juni 30, 2025, deni la Serikali lilifikia trilioni 110.05, deni la ndani likiwa TZS trilioni 35.5 na deni la nje TZS trilioni 74.55 hali iliyochangiwa na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola na ongezeko la mikopo ya nje.

DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 110.05, CAG ATAKA USHAURI UFANYIWE KAZI

Hadi kufikia Juni 30, 2025, deni la Serikali lilifikia trilioni 110.05, deni la ndani likiwa TZS trilioni 35.5 na deni la nje TZS trilioni 74.55 hali iliyochangiwa na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola na ongezeko la mikopo ya nje.

Hayo yamebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ambaye pia amesema, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepata hasara Shilingi Bilioni 3.06 kutokana na ajali za treni zilizofikia 328.

CAG ameyasema hayo wakati wa kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusema, hasara hiyo imetokana na uharibifu wa miundombinu na kupotea kwa mapato.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere.

Aidha, Kichere amesema pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeokoa TZS bilioni 14.5 kuanzia Julai 2024 hadi Juni 2025 kupitia operesheni za uchunguzi.

Amesema kati ya fedha hizo, TZS bilioni 10.1 ni fedha taslimu na TZS bilioni 4.4 ilidhibitiwa sambamba na kurejesha vifaa na mali zilizoelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yenyewe ina madeni ya kodi yanayofikia takribani TZS bilioni 7.25 ambayo yameendelea bila kukusanywa kwa zaidi ya miaka 17 na kwamba kesi za kikodi zimeongezeka kwa kasi toka saba kwa mwaka 2019/2020, hadi kufikia 1,223 kwa mwaka 2024/2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Hali hii inaashiria udhaifu katika mifumo ya utatuzi wa migogo ya kikodi, hali hii inachangia na ukosefu wa mifumo madhubuti ya usuluhishi wa mapema, ndani ya mamlaka ya mapato," amesema CAG Kichere.

Kuhusu Shirika la Reli Tanzania (TRC), lenyewe limepata hasara TZS bilioni 3.06 kutokana na ajali za treni zilizofikia 328 ambapo CAG amesema imetokana na uharibifu wa miundombinu na kupotea kwa mapato, huku akisema ushauri kuhusu masuala ya kikodi unatakiwa kufanyiwa kazi na Serikali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.