Skip to main content

DED MWARIKO AWASHUKIA MAFUNDI WAHARIBIFU, AWAPA MAAGIZO WASIMAMIZI IDARA YA ELIMU MPIMBWE

Na Daniel Gahu, Majimoto - Katavi.

DED MWARIKO AWASHUKIA MAFUNDI WAHARIBIFU, AWAPA MAAGIZO WASIMAMIZI IDARA YA ELIMU MPIMBWE

Na Daniel Gahu, Majimoto - Katavi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Bi. Shamim Mwariko, amewataka Wasimamizi wa Idara ya Elimu kuhakikisha kuna Maendeleo mazuri ya Wanafunzi katika Taaluma na Afya.

Bi. Mwariko ameyasema hayo katika Ziara yake ya kukagua miradi ya elimu katika Kata ya Majimoto,iliyofanyika kwa Lengo la kukagua kasi ya utekelezaji wa Miradi hiyo, hali ya mazingira ya wanafunzi kujifunza na mpangilio wa nyaraka mbalimbali inayohusu miradi.

Miongoni mwa Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya Majimoto inayojengwa eneo la Shule ya Sekondari Majimoto, Mradi unaogharimu kiasi cha Shilingi 342,900,000.00 kutoka chanzo cha BOOST, kwa Lengo la kujenga vyumba 8 vya Madarasa, Jengo la utawala na vyoo vya Wavulana na Waschana, ambapo Mradi huo kwa ujumla umefikia hatua nzuri ya utekelezaji.

Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Bweni Shule ya Sekondari Majimoto, na kituo cha mafunzo ya walimu (TRC), na miradi yote hiyo inalenga kuongeza weledi katika sekta ya elimu.

Aidha kiongozi huyo, alitoa Wito kwa Wasimamizi wa Miradi kuhakikisha wanalinda Rasilimali za Serikali ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua mafundi waharibifu, wanaotumia vifaa vibaya na kusababisha hasara kama vile kupasuka kwa tofali na marumaru, akibainisha kuwa usimamizi mzuri wa miradi ni chachu ya maendeleo na ustawi wa jamii ya Halmashauri ya Mpimbwe.

Nao Wakuu wa Divisheni na vitengo walioambatana na katika ziara hiyo, Wametoa ushauri kwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo, wakisisitiza utembeleaji wa mara kwa mara wa miradi, swala ambalo litasaidia kuendelea kuleta Ufanisi katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.