Skip to main content

DED BUHIGWE AAGIZA KILA KAYA KUWEKA UTARATIBU WA KUFANYA USAFI

Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imezindua kampeni ya usafi katika maeneo mbalimbali ya barabara, masoko na makazi ya wananchi, ikiwa ni mkakati wa kuzuia maafa pamoja na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El-Nino.

DED BUHIGWE AAGIZA KILA KAYA KUWEKA UTARATIBU WA KUFANYA USAFI
Studio Narration JAMBO FM

DED BUHIGWE AAGIZA KILA KAYA KUWEKA UTARATIBU WA KUFANYA USA...

0:00 --:--

Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imezindua kampeni ya usafi katika maeneo mbalimbali ya barabara, masoko na makazi ya wananchi, ikiwa ni mkakati wa kuzuia maafa pamoja na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El-Nino.

Zoezi hilo limezinduliwa katika Kata ya Mnanila, Wilaya ya Buhigwe, na kuongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, George Mbilinyi, ambaye alisisitiza umuhimu wa kila kaya kuwa na utaratibu wa kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mbilinyi alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama, hususan katika kipindi cha mvua, ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa mafuriko na magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira.

Kwa upande wao, viongozi mbalimbali walioshiriki katika kampeni hiyo, akiwemo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma, Msafiri Nzunuri, pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Manyovu, CP Abdul Mstapha, wamewataka wananchi kutambua kuwa jukumu la kuweka mazingira safi na salama ni la kila raia.

Viongozi hao walisema ushirikiano wa wananchi katika usafi wa mazingira ni muhimu katika kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mlipuko, hasa wakati wa msimu wa mvua.

Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wamepongeza hatua iliyochukuliwa na viongozi ya kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha usafi wa mazingira.

Aidha, waliiomba Halmashauri kutoa kipaumbele kwa maeneo yenye changamoto ya miundombinu, hususan barabara na maeneo mengine ambayo huwa magumu kupitika wakati wa msimu wa masika, ili yafanyiwe ukarabati kwa wakati.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.