Katika kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imetoa elimu kwa askari wa ajira mpya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza baada ya kutoa elimu hiyo iliyotolewa Julai 30, 2026, Afisa wa DCEA Kanda ya Ziwa, Jafari Mtepa amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa askari wapya, huku ikielezwa kuwa matumizi na biashara ya dawa hizo inasababisha madhara kwa jamii pamoja na kuathiri uchumi wa taifa.

Askari hao, wamesisitizwa kuwa pamoja na jukumu lao la kuokoa maisha na mali za wananchi, kama sehemu ya vyombo vya ulinzi na usalama wana wajibu wa kushiriki katika kulinda jamii dhidi ya athari za dawa za kulevya.
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa kuhusu madhara ya dawa za kulevya na nafasi yao katika kushiriki mapambano dhidi ya tatizo hilo.


Discussion
Reader comments
0 contributions