Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella, amewataka wasimamizi wa Mradi wa Ufyatuaji Matofali unaosimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuongeza kasi ya uzalishaji na kuimarisha mikakati ya kutangaza bidhaa zao ili kupanua soko na kuwafikia wateja wengi zaidi.
Wella ametoa wito huo wakati akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kutembelea mradi huo uliopo Kata ya Kitete, Manispaa ya Tabora, kwa lengo la kukagua maendeleo ya uzalishaji, utoaji wa huduma na mwenendo wa uendeshaji wa mradi.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa kuongeza mwonekano wa mradi kupitia mikakati madhubuti ya masoko, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya wateja na kuimarisha upatikanaji wa soko la matofali yanayozalishwa.
Mradi huo ni miongoni mwa shughuli zinazotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa lengo la kuzalisha matofali na kuwahudumia wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanaohitaji bidhaa hizo kwa ajili ya shughuli za ujenzi.
Discussion
Reader comments
0 contributions