Skip to main content

DC SEMINDU ATAKA ELIMU YA ARDHI ITOLEWE KWA WANANCHI KUEPUKA MIGOGORO MBULU

Na Afarah Suleiman, Mbulu - Manyara.

DC SEMINDU ATAKA ELIMU YA ARDHI ITOLEWE KWA WANANCHI KUEPUKA MIGOGORO MBULU

Na Afarah Suleiman, Mbulu - Manyara.

Maafisa ardhi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wametakiwa kutoa Elimu kwa Wananchi wa Wilaya hiyo, juu matumizi bora ya ardhi, umiliki wa ardhi pamoja na kuwapatia hati miliki za maeneo yao, ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu katika kikao cha robo tatu ya mwaka cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mbulu na kusema, migogoro mingi ya ardhi inatokana na wananchi kutokuwa na Elimu pamoja na hati miliki.

"Maafisa ardhi nendeni mkatoe elimu kwa wananchi juu ya matumiz ya ardhi," alisema Semindu.

Aidha, katika kikao hicho Semindu amepiga marufuku uchangishwaji wa wazazi na walezi michango kwa ajili ya kulipa walimu wanaojitolea katika shule mbalimbali na kumuagiza afisa Elimu kuona namna ya kufanya mgawanyo wa walimu wa waliopo kwani Serikali imeendela kutoa ajira kwa walimu.

"Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita juu ya Elimu bure ni marufuku wazazi au walezi kuchangishwa michango," alisema Semindu.

Aidha, Semindu amewataka madiwani hao wa halmashauri ya mji wa mbulu kwenda kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya ya halmashari hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Sylevester Ombay amesema wamepokea maagizo hayo na watakwenda kusimamia pamoja ukusanyaji wa mapato na matumizi ya Halmashauri.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.