Skip to main content

DC MWENDA AKAGUA MIRADI ITAKAYO TEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU

Na Saulo Stephen - Singida.

DC MWENDA AKAGUA MIRADI ITAKAYO TEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU

Na Saulo Stephen - Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda, amefanya ziara ya kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026 pamoja na kujionea maandalizi ya mapokezi ya Mwenge huo wilayani humo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenda amewapongeza watumishi, wananchi wa Wilaya ya Iramba na Halmashauri kwa maandalizi mazuri ya kuupokea Mwenge wa Uhuru. Amesema maandalizi hayo yanaonesha utayari wa Wilaya ya Iramba kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa mafanikio makubwa.

Aidha, amewahimiza wananchi wote wa Wilaya ya Iramba kujitokeza kwa wingi tarehe 24 Julai, 2026 kuupokea na kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru, akieleza kuwa tukio hilo ni fursa ya kuendelea kuhamasisha uzalendo, umoja, maendeleo na ushiriki wa wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa mujibu wa ratiba, Mwenge wa Uhuru 2026 utapokelewa katika Uwanja wa Mcharukoni, Kijiji cha Ndulungu, huku mkesha wa Mwenge ukifanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misigiri.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.