Skip to main content

DC MASINDI ATOA MAJIBU KERO ZA WANANCHI WA MWASUBI

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Peter Masindi, amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mwasubi, ukiwakutanisha wananchi wa Vijiji vya Mwasubi, Itongoitale na Ngw’anghili, ambapo amesikiliza changamoto mbalimbali na kuzitatu ikiwemo maji, barabara, elimu na huduma za afya.

DC MASINDI ATOA MAJIBU KERO ZA WANANCHI WA MWASUBI
Studio Narration JAMBO FM

DC MASINDI ATOA MAJIBU KERO ZA WANANCHI WA MWASUBI

0:00 --:--

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Peter Masindi, amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mwasubi, ukiwakutanisha wananchi wa Vijiji vya Mwasubi, Itongoitale na Ngw’anghili, ambapo amesikiliza changamoto mbalimbali na kuzitatu ikiwemo maji, barabara, elimu na huduma za afya.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU PETER MASINDI

Mkutano huo umefanyika katika Kijiji cha Ngw’anghili, ambapo wananchi wamewasilisha changamoto ya huduma ya maji pamoja na ubovu wa barabara ya Mwanamakanga–Ngw’ang’hili, huku wakieleza pia hitaji la kuwa na Shule ya Sekondari ya Kata ili wanafunzi wasilazimike kusoma katika Shule ya Sekondari Bunambiyu.

Akizungumza katika mkutano huo, DC Masindi amesema mafanikio ya mwanadamu yamebebwa na mambo manne, ambayo ni kumjua Mungu kwa kuwa ndiye mtoa baraka na neema, kuwa na ushirika na watu, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujali muda, akiwataka wananchi kuzingatia misingi hiyo katika maisha yao ya kila siku.

Kuhusu changamoto ya maji, Mha. Masindi amewasiliana kwa njia ya simu na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima, ambaye amesema Tanzania ina jumla ya vijiji 575 ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya maji, huku Wilaya ya Kishapu ikiwa na vijiji 42. Amesema kupitia Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria, kwa mwaka huu vijiji vitatu vimeanza kunufaika, ambavyo ni Itongoitale Kata ya Mwasubi, Wizunza Kata ya Mwadui Lohumbo na Mihama katika Kata ya Lagana.

handisi Kamazima amesema wakati wananchi wakisubiri utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria ambao unatarajiwa kuchukua muda, wataalamu wa survey kutoka Bonde la Kati wameingia Kijiji cha Itongoitale kwa ajili ya kutafuta chanzo cha maji, na baadaye wataendelea na Kijiji cha Ngw’anghili.

Akizungumza kuhusu barabara ya Mwanamakanga–Ngw’ang’hili, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Eliya Mgaya, amesema ni kweli barabara hiyo imeharibika kwa kiasi kikubwa, huku akieleza kuwa mipango ipo katika taratibu za manunuzi ya awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwezi Desemba 2026. na kuanisha kuwa ukarabati utafanyika katika maeneo yenye changamoto kubwa kwa kuweka vifusi na mawe ili kurejesha hali ya barabara hiyo.

DIWANI WA KATA YA MWASUBI SAMSON GELEWA

Diwani wa Kata ya Mwasubi, Mhe. Samson Gelewa, amesema Serikali tayari imeipatia Kata hiyo kiasi cha Sh milioni 603 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata katika Kijiji cha Ngw’ang’hili, fedha ambazo zitatumika kujenga vyumba nane vya madarasa, matundu 11 ya vyoo, jengo la utawala, jengo la TEHAMA na maabara.

Diwani Gelewa amesema wananchi pia wameendelea kushiriki katika ujenzi wa huduma za afya kwa kujenga boma la zahanati, huku Ofisi ya Mbunge ikiwawezesha kwa kutoa mbao 100 na mabati 70 kwa ajili ya upauaji wa jengo moja. Amesema wananchi wamechangia fedha za kumlipa fundi, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu tayari imeweka bajeti ya Sh milioni 35 kwa ajili ya zahanati hiyo.

Amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutafanya Kata ya Mwasubi yenye vijiji vitatu kubakiwa na Kijiji kimoja kisicho na zahanati, huku wananchi wakiendelea na jitihada za kuhakikisha huduma za afya zinaimarika na hatimaye wanapata kituo cha afya katika kata hiyo.

MRATIBU WA MAAFA HALIMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU ROBERT MHINA

Kupitia mkutano huo Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Robert Mhina, ametoa elimu kuhusu maandalizi na tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño na jinsi ya kuchukua hatua za kujikinga, huku Serikali ikisisitiza kuwa ushirikiano wa karibu kati yake na wananchi ni muhimu katika kutatua changamoto za maendeleo na kukabiliana na majanga.

Kwa upande wao baadhi ya wanachi waliojitokeza kuwasilisha kero zao kwa mkuu huyo wa wilaya wameishukuru seriakali kwa kufika katika eneo hilo na kutoa suluhisho la changamoto zao huku wakitaka utaratibu huo kuwa endelevu na mara kwa mra

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.