
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vincent Mashinji, amezindua rasmi mradi wa maji katika Kijiji cha Simbanguru, Tarafa ya Nkonko, kupitia ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali la World Save International, ikiwa ni sehemu ya kuboresha na kusogeza huduma bora kwa Wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Mashinji amesema ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo una mchango mkubwa katika kuharakisha upatikanaji wa huduma muhimu, hususan maji safi na salama huku akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya aliambatana na Afisa Tarafa ya Nkonko, Yahaya Njiku, ambaye aliwataka wananchi wa Simbanguru kuitunza na kuilinda miundombinu ya mradi huo ili uweze kudumu na kuendelea kunufaisha jamii ya sasa na vizazi vijavyo.Viongozi wengine walioshiriki Ziara hiyo ni Pamoja na Diwani wa kata ya Isseke,Wataalamu na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya tawi la kata.
Mradi huo unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Kijiji cha Simbanguru na maeneo ya jirani, hatua itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Tarafa ya Nkonko.
Discussion
Reader comments
0 contributions