Skip to main content

DC MAGWAZA AZITAKA NGOs KUSHIRIKIANA NA SERIKALI UTOAJI HUDUMA ZA KIJAMII

Na Tryphone Odace, Kibondo – Kigoma.

DC MAGWAZA AZITAKA NGOs KUSHIRIKIANA NA SERIKALI UTOAJI HUDUMA ZA KIJAMII

Na Tryphone Odace, Kibondo – Kigoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Kanali Mstaafu Aggrey Magwaza, ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kuendelea kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za kijamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Magwaza ameyasema hayo wakati wa kikao na wawakilishi wa mashirika hayo kilicholenga kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano na kuongeza mchango wa NGOs katika maendeleo ya jamii wilayani Kibondo.

Amesema, “ushirikiano kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia programu na miradi mbalimbali ya maendeleo ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.”

DC Magwaza amesema, mashirika hayo yana mchango mkubwa katika kusaidia Serikali kufikia malengo yake ya maendeleo, hususan katika maeneo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

“Ushirikiano kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na fursa za maendeleo,” amesema Magwaza.

Kwa upande wao, baadhi ya wawakilishi wa mashirika hayo wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali wilayani Kibondo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Wamesema wataendelea kuweka nguvu katika maeneo muhimu ikiwemo elimu, utoaji wa ujuzi na programu zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Hatua hiyo inakuja wakati mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yakiendelea kutekeleza programu na miradi wilayani Kibondo, hususani ile inayokwenda sambamba na mikakati na vipaumbele vya Serikali.

Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.