Skip to main content

DC KAWAWA AHIMIZA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI, AWATAJA WALEMAVU

Watendaji wa Vijiji Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, wametakiwa kutoa huduma bora kwa Wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu, ili kujenga imani katika jamii.

DC KAWAWA AHIMIZA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI, AWATAJA WALEMAVU
Studio Narration JAMBO FM

DC KAWAWA AHIMIZA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI, AWATAJA W...

0:00 --:--

Watendaji wa Vijiji Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, wametakiwa kutoa huduma bora kwa Wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu, ili kujenga imani katika jamii.

Wito huo, umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang', Vita Kawawa wakati akifungua mafunzo kuhusu utawala bora, Demokrasia na Haki za binadamu kwa Watendaji wa Vijiji wa Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Prosper Kiasinini, amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha watendaji wajibu wao katika kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo Manyara ukiwa ni mkoa 19 kupatiwa mafuzo hayo.

Nao baadhi ya Watendaji waliopatiwa mafunzo hayo wameishukuru Wizara wakisema watakwenda kusimamia vyema Wananchi hasa wenye mahitaji maalum.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.