Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda Leo amefanya Ziara ya Kikazi katika Kijiji cha Orng'adida na Kusikiliza Kero mbalimbali kutoka kwa Wananchi wa Kijiji hicho na Vijiji jirani vya Kata ya Qash na Galapo.
Wakati wa uwasilishwaji wa Kero hizo, Wananchi walijitokeza na kusema Kero zao ambazo asilimia kubwa ya kero hizo ni Migogoro ya Ardhi baina ya Kijiji na Wananchi, Uuzaji wa Ardhi kiholela, Changamoto ya Barabara, Umeme na Ukosefu wa Maadili Kwa vijana kutokana na Madawa ya kulevya na Ukosefu wa malezi mazuri ya Wanamama Kwa watoto wao kutokana na Ulevi.

Baada ya Kusikiliza Kero hizo, DC Kaganda pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya walibaini Migogoro mingi ya Ardhi katika Kijiji hicho imetokana na uongo wa kufoji kwa nyaraka za Hati ya Makubaliano na makabidhiano ya maeneo hayo huku viongozi wa Halmashauri ya Kijiji wakitumika vibaya katika kufanya maamuzi ya Migogoro hiyo.
Aidha, DC Kaganda ameitaka Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Kuchunguza mtandao wote ambao Mwenyekiti wa Kijiji ameungana nao katika Uuzaji wa Ardhi kiholela huku Mwenyekiti huyo akisimamishwa Kwa muda wakati Uchunguzi huo Ukiendelea.

DC Kaganda pia amekitaka Kijiji kuwarudishia Wananchi wote walionyang'anywa Ardhi zao kimakosa na wale ambao walikutwa na nyaraka za kufoji wameshikiliwa na Jeshi la polisi Kwa ajili ya Uchunguzi na kuchukuliwa Hatua za Kisheria Kwa kuidanganya Serikali.





Discussion
Reader comments
0 contributions