Skip to main content

DC KAGANDA AIASA JAMII KUTENDA YALIYO MEMA

Jamii imetakiwa kuendelea kutenda matendo mema wakati wote hata baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani na kwaresma ili kuwa na jamii yenye hofu ya mwenyezi mungu .

DC KAGANDA AIASA JAMII KUTENDA YALIYO MEMA

Jamii imetakiwa kuendelea kutenda matendo  mema  wakati wote hata baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani na kwaresma ili  kuwa na jamii yenye hofu ya mwenyezi mungu .

Wito huo, umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda wakati  wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Manyara iliyoambatana na utoaji wa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Hosana cha mjini Babati.

Naye Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Bahati Haule amesema ni vyema jamii ikashiriki  kutenda  matendo mema yanayompendeza Mungu, ikiwa ni pamoja na  kufichua  vitendo vya rushwa.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Hossana, Neema Munis ameishukuru TAKUKURU kwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.