Mkuu wa Wilaya ya Babati, Hashimu Mgandilwa, amewataka Wenyeviti wa serikali za mitaa na Vijiji ndani ya wilaya hiyo, kuepuka kukaa ofisini kwa muda wote bila sababu za msingi.
Aidha, Mgandilwa amesema badala yake wajishughulishe na kazi zingine za uzalishaji mali na utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, Watendaji wa Mitaa na Vijiji, pamoja na Watendaji wa Kata, katika kikao kilicholenga kuwakumbusha majukumu yao na kuweka uelewa wa pamoja.

- Mkuu wa Wilaya ya Babati, Hashimu Mgandilwa.
Lengo la kikao hiko lilikuwa ni kuepusha mkanganyiko kwa Wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema, wakati wa kuwania nafasi hizo, viongozi hao walitakiwa kuwa na shughuli nyingine za kujipatia kipato, hivyo si sahihi kwa baadhi yao kutaka kukaa ofisini kuanzia wakati wa kufunguliwa hadi kufungwa kwa ofisi, kwani kufanya hivyo si sehemu ya majukumu yao ya kila siku.
“Wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa serikali za mitaa, nafikiri ni jambo ambalo tunalifahamu wakati wa uchukuaji wa fomu ambazo zimetupa nafasi hizi ambazo tunazitumikia"
"Fomu ile ilitutaka tuwe na shughuli nyingine za kujipatia kipato, sasa wapo wenyeviti ambao wanataka ofisi inapofunguliwa awepo ofisini mpaka inafungwa, si kazi yenu,” amesema DC Mgandilwa.
Discussion
Reader comments
0 contributions