Mwanasoka Mohamed Damaro Camara, kiungo aliyewahi kutamba na Klabu za Singida Black Stars na Yanga SC, ametangaza kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars.
Mbali na kuvunja mkataba, Damaro pia ameukana uraia wa Tanzania akidai inatokana na sababu binafsi na zile za kifamilia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Damaro ameandika- "Habari Mabibi na Mabwana, kwa heshima naangaza kuvua uraia wangu wa Tanzania niliyopewa,"
"Hivyo naukana kwa sababu zangu binafsi na za kifamilia, na kwa heshima natangaza kusitisha mkataba wangu na Singida Black Star. Asante."
Discussion
Reader comments
0 contributions