Skip to main content

CRDB KUDHAMINI MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

CRDB KUDHAMINI MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Benki ya CRDB inatarajia kudhamini maonyesho makubwa ya mifugo kwa kanda ya ziwa yatakayaofanyika Mei 30 - 31, 2026 katika mkoa wa Shinyanga yakilenga  kufungua fursa zaidi kwa wafugaji na pia kutatua changamoto za kufuga Wakati huu ambao wafugaji wengi wanakabiliwa na upungufu wa utaalamu wa kisasa jambo linalosababisha mifugo kufa na kupata hasara.

Akizungumzia maonyesho hayo   meneja wa CRDB kanda ya magharibi  Wambura Wagana amesema Benki hiyo imedhamini maonesho hayo na kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 20 kama wadhamini wakuu wa maonesho hayo huku akiwashauri wafugaji kukata bima ya mifgugo ili kutatua changamoto ya kupata hasara.

Aidha  Wagana Wambura amesema Benki ya CRDB imeingia mkataba na chama cha wafugaji nchini kuwakopesha wakulima mikopo yenye riba nafuu ili kuwainua kiuchumi wafugaji huku akiwahimiza wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.

Amesema katika kipindi chote cha maonesho hayo Benki ya CRDB itakuwa pale muda wote kuhakikisha kwamba inawafungulia fursa ya kupata mtaji wafugaji wa aina zote na wanaofuga ng’ombe, mbuzi, kuku na Wanyama wengine lengo likiwa ni kuhakikisha kila anayehusika na kujongea kutafuta fursa hiyo anafikiwa kikamilifu nakupatiwa kile anachohitaji.

Naye muandaaji wa maoneshio hayo  Charles Nduku kutoka kampuni ya Farm Flex group amesema Maonesho haya yanatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya ufugaji na kuboresha uchumi wa wakazi wa kanda hiyo yatachagizwa na mashindano ya michezo mbalimbali ukiwemo mchezo maarufu kanda ya ziwa wa mbio za baiskeli.

Aidha amesema katika maonesho hayo wataalikwa wataalamu mbalimbali watakaotoa elimu ya ufugaji wa kibisashara ili wafugaji wajifunze mbinu za kufuga kisasa na kukidhi soko la kimataifa.

Akionesha mfano kuwa mfugaji anaweza kufuga ng’ombe wengi kiholela bila kupata mafanikio kwa kuuza kwa bei ndogo ng’ombe mmoja kwa shilingi laki mbili mpaka tatu lakini kwenye manesho hayo akajifunza kufuga mifugo wachache kitaalamu na akauza ng’ombe mmoja kwa shilingi milioni moja hadi mbili na kupata faida ya kutosha.

Hata hivyo ameenda mbali zaidi akiangazia ufugaji wa mataifa mengine na masoko ya kimataifa kuwa kwa kawaida walaji wa maeneo hayo wananunua kitoweo cha nyama au bidhaa zingine zitojanazo na mifugo kwa kufuata historia ya Wanyama hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.