Skip to main content

CR7 NA MWISHO WA ENZI KIMATAIFA! RONALDO ASTAAFU URENO

Mwisho wa enzi umefika.

CR7 NA MWISHO WA ENZI KIMATAIFA! RONALDO ASTAAFU URENO

Mwisho wa enzi umefika.

Mwanasoka nguli, Cristiano Ronaldo - CR7 ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa baada ya miaka 23 akiitumikia timu ya taifa ya Ureno.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 41, ametangaza uamuzi huo kupitia video ndefu aliyoiweka kwenye mitandao yake ya kijamii, Alhamisi hihii.

Anasema, "siku imefika ya kuirudisha jezi namba 7 ya timu yetu ya taifa. Sikuwahi kuhisi ni yangu peke yangu. Lakini kwa miaka 23 nilipata heshima na jukumu la kuivaa, kuitetea na kuibeba kwenye viwanja kote duniani."

CR7 akaongeza kuwa, "Leo, wakati umefika wa kuikabidhi kwa kizazi kijacho.

Kiuhalisia Ronaldo anamaliza safari yake akiwa na rekodi ambazo huenda zisitavunjwa kamwe:

Mechi:

234 - Rekodi ya juu zaidi duniani kwa mchezaji wa kiume

Magoli:

146 - Mfungaji bora wa muda wote kwenye soka la kimataifa

Mataji:

Euro 2016, Nations League 2019 na 2025

Safari yake ilianza Agosti 2003 akiwa na umri wa miaka 18 tu, dhidi ya Kazakhstan. Na mechi yake ya mwisho ilikuwa Septemba mwaka huu, ushindi wa 1-0 dhidi ya Wales.

Kustaafu huku kunakuja baada ya ugomvi wake na kocha mpya Jorge Jesus, ambaye alimweka benchi kwenye mechi dhidi ya Norway na Ronaldo akaondoka kambini, kitendo kilichomfanya afungiwe siku 30 na Shirikisho la Soka la Ureno.

KUMBUKA:

Ronaldo hajastaafu soka kabisa. Bado ataendelea kuichezea Al Nassr ya Saudi Arabia, akiwa amebakiza magoli 15 tu kufikisha magoli 1000 kwenye karier yake.

Kumbukumbu ya kauli hii itabaki kichwani mwa wapenda soka hada mashabiki zake, "Leo safari yangu uwanjani na timu ya taifa inakwisha. Naondoka kichwa juu, nikiwa na fahari. Lakini kamwe sitaacha kuwa mmoja wenu. Ureno itabaki moyoni mwangu milele."

MWISHO WA ENZI YA CR7 NA SIUUUU!

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.