Skip to main content

CP MKAMA: POLISI JAMII WASIKILIZE, WATATUE KERO ZA WANANCHI KATIKA VIPINDI VYOTE

Na Saada Almasi, Bariadi – Simiyu.

CP MKAMA: POLISI JAMII WASIKILIZE, WATATUE KERO ZA WANANCHI KATIKA VIPINDI VYOTE

Na Saada Almasi, Bariadi – Simiyu.

Kamishna wa Polisi kutoka Kamisheni ya Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, CP Alex Mkama amewataka Polisi kata katika maeneo yote ya mkoa wa Simiyu, kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri kati yao na jamii inayowazunguka, ili kuweza kutambua na kutatua kero zao katika vipindi vyote.

CP Mkama ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu, kilichofanyika mjini Bariadi na kusema, uhusiano mzuri unapokuwepo kati ya jamii na polisi vitendo viovu ni rahisi kupungua.

“Tengenezeni usikivu mzuri wa kero za wananchi ,shirikianeni katika nyakati nzuri na mbaya maana kuna nyakati ambazo ni za huzuni kama misiba hebu ingieni huko mshiriki kwa kujitolea muwe sehemu ya maisha yao hii itaongeza ukaribu watawaona kuwa ni sehemu yao na matukio ya kihalifu yatapungua,” amesema  CP Mkama.

Ameongeza  kuwa, Polisi Jamii ni muhimu kuwa karibu na wananchi kwa sababu wananchi ambao wana taarifa nyingi kuhusiana na matukio yote yanatokea katika maeneo yao, hivyo watumie nafasi hiyo kwa uadilifu.

Aidha, CP Mkama pia amewataka askari hao kuzingatia maboresho ndani ya jeshi hilo ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi na kuleta matokeo chanya katika ulinzi na usalama wa nchi.

Kikao kazi cha jeshi hilo ni muendelezo wa vikao vingine vinavyolenga kutathimini utekelezaji na usimamizi wa majukumu ya kamisheni hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.