Skip to main content

CP HAMDUNI, PAMBA JIJI FC WATETA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi pamoja na wachezaji wa Timu ya Pamba Jiji FC katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na timu hiyo pamoja na kuhamasisha maendeleo ya soka mkoani Mwanza.

CP HAMDUNI, PAMBA JIJI FC WATETA
Studio Narration JAMBO FM

CP HAMDUNI, PAMBA JIJI FC WATETA

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi pamoja na wachezaji wa Timu ya Pamba Jiji FC katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na timu hiyo pamoja na kuhamasisha maendeleo ya soka mkoani Mwanza.

Katika mazungumzo hayo, CP Hamduni ameipongeza timu ya Pamba Jiji FC kwa jitihada zake za kupeperusha bendera ya Mwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na kueleza kuwa mafanikio ya timu hiyo ni fahari kwa wakazi wote wa Mwanza. Amesema mkoa uko tayari kuwa bega kwa bega na timu hiyo ili kuhakikisha inafikia malengo yake ya kimichezo na kuleta heshima zaidi kwa mkoa.

Aidha, CP Hamduni ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kutoka Ofisi yake kwa uongozi na wachezaji wa Pamba Jiji FC, ikiwa ni pamoja na kuisaidia timu hiyo kupata wadhamini na kuimarisha miundombinu yake ya michezo. Amesisitiza kuwa serikali ya mkoa inatambua mchango mkubwa wa michezo katika kukuza uchumi, ajira kwa vijana na kudumisha umoja miongoni mwa wananchi.

Sambamba na hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi na wachezaji wa Pamba Jiji FC kuendelea kudumisha mshikamano, nidhamu ya hali ya juu na kujituma katika majukumu yao ya kila siku. Amewakumbusha kuwa nidhamu na umoja ndio msingi mkuu wa mafanikio ya timu yoyote duniani, na kwamba wanapaswa kuwa mfano bora kwa vilabu vingine hapa nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.