Skip to main content

CONGO YATANGAZA DHARURA YA KITAIFA

Congo (DRC) kushuhudia Bendera kupepea nusu mlingoti kwa muda wa siku tatu mfululizo.

CONGO YATANGAZA DHARURA YA KITAIFA
Studio Narration JAMBO FM

CONGO YATANGAZA DHARURA YA KITAIFA

0:00 --:--

Congo (DRC) kushuhudia Bendera kupepea nusu mlingoti kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Imetangaza dharura ya kitaifa Bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku 3 ikiwa ni katika kuomboleza

Wahanga wa ajali ya ndege iliyoua watu 17, wakiwemo maafisa waandamizi wawili kutoka mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo.

Taarifa ya ikulu ya Rais Félix Tshisekedi (Palais De la Nation) mjini Kinshasa imeeleza kutolewa kwa agizo hilo la dharura huku likianza kutekelezwa siku yah ii leo Jumatatu ya Sept.28 hadi pale miili ya wahanga itakapo zikwa.

Aidha taarifa ya Jeshi imebainisha waliofariki ni pamoja Luteni Jenerali Joseph Mutombo Katalayi Tiende, Rais wa Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Congo, Luteni Jenerali Lucien-René Likulia Bakumi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kijeshi wa Jeshi la Congo (FARDC), pamoja na wajumbe kadhaa wakiwa na wasaidizi wao.

Kufuatia hilo Serikali ya Congo pia imewataka wananchi wa Taifa hilo kuwa watulivu Wakati mchakato wa shughuli za mazishi ya ukiendelea.

Ajali hiyo ya ndege iliyotajwa kuwa mbaya nchini Congo ilitokea siku ya ijumaa ya sept.25 kando na mji wa Kenge ulio makao makuu ya jimbo la Kwango,

Ambayo imehusisha ndege ya LET 410 UVP iliyokuwa ikiendeshwa na shirika la ndege la TRACEP Congo Aviation.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi, ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Kikwit kuelekea Kinshasa ilipopata hitilafu ya kiufundi na kujaribu kuelekezwa katika eneo hilo la Kenge.

Hata hivyo, mamlaka za eneo hilo zilisema hakukuwa na uwanja wa ndege unaofanya kazi kwa ajili ya kutua, hivyo ndege ilianguka katika eneo la makazi kabla ya kulipuka na kushika moto.

Kadharika Wizara hiyo ilisema watu wote 17 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, abiria 13 na wahudumu wanne, walifariki dunia. Awali idadi ya vifo ilikuwa imetajwa kuwa 13 kabla ya kuongezwa baada ya operesheni za uokoaji kukamilika.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi, Jean-Pierre Bemba, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa cheti cha uendeshaji wa ndege (Air Operator Certificate) cha TRACEP Congo Aviation hadi uchunguzi rasmi wa ajali hiyo utakapokamilika. Hatua hiyo inasimamisha shughuli zote za shirika hilo nchini Congo huku Serikali ikisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.