Skip to main content

CIVISCE YAWAPATIWA VIFAA WAFANYABIASHARA WADOGO KIGOMA.

Wafanyabiashara wadogo katikaa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameaswa kutumia vyema fursa za kiuchumi zinazowazunguka ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujipatia maendeleo endelevu kwa ustawi wa jamii.

CIVISCE YAWAPATIWA VIFAA WAFANYABIASHARA WADOGO KIGOMA.

Wafanyabiashara wadogo katikaa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wameaswa kutumia vyema fursa za kiuchumi zinazowazunguka ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujipatia maendeleo endelevu kwa ustawi wa jamii.

Mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bi. Thabitha Everist Mkilamweni, amesema hayo wakati kizungumza na Jambo FM, mara baada ya hafla ya ugawaji wa vifaa kwa wafanyabiashara wadogo iliyoandaliwa na Taasisi ya Clear Vision For Change - CIVISCE kwa kushirikiana na Women in Africa Venturing Education - WAVE.

Bi. Mkilamweni amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo la kuwainua wanawake wajasiriamali ili waweze kufikia malengo katika shughuli zao za kila siku.

Naye mjumbe wa Baraza la uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  Tanzania Alex Luoga amesema mashirika yasikuwa ya kiserikali yataendelea kuwawezesha wanawake wajariamali kufikia malengo katika uzalishaji mali.

Kwa upande wake,  Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Clear Vision For Change, Bw. Mapendano Nabulizi, amesema vifaa hivyo vimetolewa kama mtaji wa kuanzia ili kuwawezesha kiuchumi wanawake hao.

Baadhi ya wanawake wajariamali waliopata vifaa hivyo wamesema vitawasaidia kupanua na kukuza biashara zao.

Vifaa hivyo vimetolewa baada ya wajariamali wanawake  kupatiwa mafunzo ya siku tano na Taasisi ya Clear Vision for Change yakiyolenga kuwajengea uwezo wa usimamizi wa fedha na ujasiriamali na vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Incubator, friza, na maderi ya kuhifadhia samaki.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.