SINGIDA
Maafisa wa Jeshi kutoka nchi saba za Afrika pamoja na India ambao ni wakufunzi na wanafunzi wa chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania kundi la 41/2026 wamefanya Ziara katika Kijiji cha Nyuki kilichopo Kisaki Mkoani Singida, kwa lengo la kujifunza ,shughuli za uzalishaji wa asali,Mazaonya nyuki pamoja na historia ya eneo hilo.
Ziara hiyo imefanyika Oktoba 13, na kuongozwa na Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania, ambaye pia ni mkuu wa msafara huo Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande, na Kupokelewa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki Philemon Kiemi. 
Akizungumza na Jambo Media wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki, Philemon Kiemi, amesema maafisa hao wamefurahishwa na fursa ya kujifunza historia ya kijiji hicho pamoja na umuhimu wa zao la asali, ikiwemo bidhaa inayojulikana kama Vumbi la Singida.
Kiemi amesema Kijiji cha Nyuki ni miongoni mwa maeneo yenye historia na utambulisho wa asili wa Mkoa wa Singida, hivyo ametoa wito wa kuendelezwa na kuhifadhiwa kwa eneo hilo ili liendelee kuwa kivutio muhimu cha kiutamaduni na kiuchumi pia.
Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki Philemon Kiemi akieleza kuhusu uzalishaji wa Mazao ya Nyuki, kwa Wakufunzi na Wanafunzi wa Ukamanda na Unadhimu Kundi la 41/2026 walipotembelea katika Makao makuu ya Kijiji cha Nyuki, Kisaki Mkoani Singida
Katika ziara hiyo, maafisa hao wametembelea maeneo mbalimbali ya Kijiji cha Nyuki na kujionea urithi wake wa asili, ikiwa ni sehemu ya mafunzo yenye mada isemayo “Economic Development for National Security”, inayosisitiza uhusiano kati ya maendeleo ya kiuchumi na usalama wa taifa.
Discussion
Reader comments
0 contributions