Skip to main content

CHIWELESA AKABIDHI MILIONI 8.5 KUIWEZESHA KIUCHUMI UVCCM BIHARAMULO

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera.

CHIWELESA AKABIDHI MILIONI 8.5 KUIWEZESHA KIUCHUMI UVCCM BIHARAMULO

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Ezra John Chiwelesa, ametimiza ahadi yake ya kuiwezesha kiuchumi Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Biharamulo kwa kukabidhi jumla ya shilingi milioni 8.5 kwa viongozi wa UVCCM ngazi ya kata kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo na kujiongezea kipato.

Akikabidhi fedha hizo leo Julai 9, 2026, Mhe. Chiwelesa alisisitiza kuwa maendeleo ya kisiasa yanapaswa kwenda sambamba na maendeleo ya kiuchumi, akieleza kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo kujijengea uwezo wa kiuchumi huku wakiendelea kuimarisha chama.

Akizungumza baada ya kupokea fedha hizo kwa niaba ya UVCCM, Katibu wa CCM Wilaya ya Biharamulo, Cde. Adam Soud, alimpongeza Mbunge Chiwelesa kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mtaji huo.

Alieleza kuwa kila kata imekabidhiwa shilingi 500,000 kwa ajili ya kuanzisha miradi ya uzalishaji, huku akiahidi kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha zinafikia malengo yaliyokusudiwa na kuwanufaisha vijana.

Kwa upande wake, Mlezi wa UVCCM Wilaya ambaye pia ni Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Wilaya ya Biharamulo, Cde. Edina Busu, aliwataka vijana kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Aliwasisitiza kutumia fedha walizopokea kama chachu ya maendeleo na njia ya kuimarisha mshikamano ndani ya jumuiya, badala ya kuzitumia kwa namna inayoweza kuleta migawanyiko.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uwezo wa kiuchumi wa vijana wa UVCCM katika ngazi ya kata, ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na kuchangia maendeleo ya jamii pamoja na chama.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.