Na William Bundala, Ushetu - Kahama.
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amejitolea kulipia chumba cha kulala wageni muda wote wa mradi ili mkandarasi anayesimamia awe karibu na eneo la mradi la ujenzi wa kituo cha afya Ulowa kwa lengo la kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Mh Cherehani ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambapo amesisitiza kuwa fedha za mradi tayari zimetolewa hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha utekelezaji wake.

“Tunachohitaji jengo kukamilika kwa wakati,pes azote za ujenzi serikali imeshaweka sasa haina sababu ya kusuasua,nikuombe injinia kama unatoka mbali tafuta nyumba ya kulala wageni ukae hadi mradi utakapoisha na gharama zote nitalipia mimi” Amesema Cherehani.
Sambamba na hayo cherehani ameongeza kuwa katika ujenzi huo kila mmoja atimize wajibu wake,na kwamba kila fundi ana kipande chake kwahiyo kila mtu asimamie eneo lake la ujenzi ili kituo kianze kazi katika kata ya Ulowa.

“Kila mtu atimize wajibu wake,kila fundi ana kipande chake ni jukumu la kila mmoja kusimamia eneo lake ili ujenzi wa kituo hiki ukamile haraka na kamati ya siasa ya kata nanyi mna kipande chenu kuhakikisha wanasimamia vyema miradi ya maendeleo” Amengoza Cherehani.
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri hiyoo amehaidi kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya afya ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.

“Tunaishukuru serikali kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya,nakuhaidi kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya afya ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ianze kuwasaidia wananchi” Amesema Dkt
Katika taarifa iliyosomwa mbele ya Mh Cherehani kituo cha afya Ulowa kitagharimu kiasi cha shilii 657,290,391 na unahusisha ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD),Jengo la kulaza wagonjwa Pamoja na vyoo.

Discussion
Reader comments
0 contributions