Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Tanzania hakuna ugaidi na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote aliye juu ya Sheria na cheo cha mtu si kinga ya kufanya makosa ya kijinai.
Katambi ameyasema hayo hii leo Julai 29, 2026 Visiwani Zanzibar, wakati akitolea ufafanuzi taarifa zinazosambaa kuhusu Sheria ya Kuzuia Ugaidi, akisema inazuia yeyote kutishia, kupanga, kuratibu au kutekeleza vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa Wananchi.

Amesema, Serikali kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama itaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao na kuwahakikishia Wananchi kuendelea na shughuli kwa amani.
Katambi pia amesema, licha ya Tanzania kutokuwa na matukio makubwa ya ugaidi, bado upo uwezekano wa kuwepo kwa viashiria vya vitendo vya kigaidi.
Discussion
Reader comments
0 contributions