Skip to main content

CHANJO YA POLIO KUWANUFAISHA ZAIDI YA WATOTO 542,000 SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

CHANJO YA POLIO KUWANUFAISHA ZAIDI YA WATOTO 542,000 SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

Takribani watoto 542,041 wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio katika Halmashauri zote saba za mkoa wa Singida ambapo Serikali imepanga kutekeleza zoezi maalum la utoaji wa chanjo ya matone ya novel Oral Polio Vaccine type 2 (nOPV2) kwa watoto chini ya miaka 10 ili kuimarisha kinga dhidi ya kirusi hicho kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu kwa watoto.

Hayo yameelezwa leo Machi 14, 2026 katika kikao cha uhamasishaji wa kampeni ya chanjo ya Polio kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, kikihusisha viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa, wilaya pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujiandaa na utekelezaji wa kampeni hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ugonjwa wa Polio ambao unaweza kusababisha kupooza kwa viungo na hata kifo kwa watoto.

Aidha, wananchi wamehimizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Polio kwa kuwahi katika vituo vya afya pale mtoto anapoonyesha dalili za kupooza ghafla, kutoa taarifa mapema kwa wahudumu wa afya au kupiga simu namba 199 bila malipo.

Kingine ni kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vyoo ipasavyo pamoja na kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote kulingana na ratiba ya kitaifa ya chanjo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, zoezi la utoaji wa chanjo litafanyika kwa awamu mbili ambapo dozi ya kwanza itatolewa kuanzia tarehe 24 hadi 27 Machi, 2026, huku dozi ya pili ikitarajiwa kutolewa kuanzia tarehe 07 hadi 10 Mei, 2026.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.