Skip to main content

CHANGAMOTO UPOTEVU WA MAZAO KWENYE MAGHALA IMEPUNGUA - WRRB

Na Gideon Gregory - Dodoma.

CHANGAMOTO UPOTEVU WA MAZAO KWENYE MAGHALA IMEPUNGUA - WRRB

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Changamoto ya upotevu wa mazao kwenye maghala imeendelea kupungua nchini kufuatia kuimarishwa kwa usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, huku matumizi ya bima na minada ya kidijitali yakitajwa kuongeza usalama wa mazao na uwazi katika biashara.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 31, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu amesema hatua hizo zimeongeza imani ya wakulima katika mfumo huo na kupunguza kwa kiwango kikubwa upotevu wa mazao.

Amesema Kamati za Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala zimeimarishwa na zinafuatilia mazao tangu yanapowasili ghalani hadi yanapouzwa mnadani. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu.

"Mazao yote yanayohifadhiwa kwenye mfumo huo yamewekewa bima dhidi ya majanga kama moto, wizi na hasara nyingine zinazoweza kujitokeza, endapo upotevu unatokea, mhusika hulipwa fidia, huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo cha tatizo na pale panapobainika uzembe au ukiukwaji wa taratibu, hatua za kinidhamu na kisheria huchukuliwa dhidi ya wahusika,"amesema.

Mbali na usalama wa mazao, amesema mfumo huo umeongeza uwazi katika uuzaji kupitia minada ya kidijitali, wakulima na wanunuzi wanaweza kufuatilia mchakato wa mnada na kuona bei zinazopatikana, jambo linaloongeza uaminifu na kuondoa malalamiko yaliyokuwa yakijitokeza hapo awali.

"Serikali pia inaendelea kufanya tathmini ya viwango vinavyokubalika vya unyevu kwenye mazao kama korosho ili kuhakikisha ubora wa mazao unalindwa bila kuwaumiza wakulima au wanunuzi,"amesema.

Mazungumzo na vyombo vya habari hii leo Julai 31, 2026 jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, mfumo wa Stakabadhi za Ghala unaendelea kupanuliwa kwenye maeneo mbalimbali nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha biashara ya mazao inakuwa ya kisasa, yenye ushindani na inayowawezesha wakulima kupata sehemu kubwa zaidi ya thamani ya mazao yao kulingana na bei za soko la kimataifa.

Kwa sasa, matarajio ni kwamba maboresho yanayoendelea yataongeza imani ya wakulima, kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta ya kilimo na kuifanya biashara ya mazao kuwa salama, yenye uwazi na yenye manufaa kwa wadau wote.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.