Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Shelui, wilayani Iramba mkoani Singida, zimezinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, huku akimnadi mgombea wa nafasi hiyo, Omar Kinota, anayeomba ridhaa ya wananchi kuiongoza kata hiyo.
Kinota anawania nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Shelui, Agness Nasania, aliyefariki dunia mwezi Mei mwaka 2026, ambapo Kinota ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani wa Iramba pindi atakapochaguliwa kuwa diwani, ili aweze kushirikiana nao katika kutekeleza majukumu ya kuongoza kata hiyo.
Mgombea Udiwani kata ya Shelui kupitia CCM Oma Kinota akionba kura akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata
Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jonathan Mabihya, amewaomba wananchi wa Shelui kumchagua Omar Kinota ili awe diwani wa kata hiyo
Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026, ambapo wananchi wa Kata ya Shelui watapata fursa ya kumchagua mwakilishi wao katika nafasi hiyo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Jonathan Mabihya akimuombea kura Mgombea Udiwani kata ya Shelui Omar Kinota.
Discussion
Reader comments
0 contributions