Skip to main content

CCM SINGIDA YATAKA MASUALA YA ARDHI YASIMAMIWE KWA KUZINGATIA SHERIA IKIWATAJA WENYEVITI WA MITAA, VITONGOJI

Na Saulo Stephen - Singida.

CCM SINGIDA YATAKA MASUALA YA ARDHI YASIMAMIWE KWA KUZINGATIA SHERIA IKIWATAJA WENYEVITI WA MITAA, VITONGOJI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Lucia Mwiru, amewataka wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vitongoji kuhakikisha wanasimamia masuala ya ardhi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuepusha migogoro inayoweza kuvuruga amani katika jamii.

Akizungumza akiwa Mgeni Rasmi katika kikao cha wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vitongoji wa Wilaya ya Singida Mjini, Mwiru amesisitiza kuwa uuzaji wa maeneo bila kufuata taratibu za kisheria umekuwa chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo, hivyo viongozi hao wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzuia vitendo hivyo.

Mwiru amesema ni wajibu wa viongozi wa ngazi za chini kusimamia kwa umakini masuala yote yanayohusu umiliki na uhamishaji wa ardhi, huku wakihakikisha maamuzi yanayofanyika yanazingatia mamlaka husika na sheria zilizopo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Lucia Mwiru.

Aidha, amewahimiza viongozi hao kuwa walinzi wa amani, haki na maendeleo ya wananchi kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima katika maeneo wanayoyaongoza.

Kikao hicho kimewakutanisha wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vitongoji kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Singida Mjini kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi, usimamizi wa shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.