Skip to main content

CCM SINGIDA MJINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI MANISPAA

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Manispaa ya Singida, ikieleza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa kwa vitendo.

CCM SINGIDA MJINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI MANISPAA
Studio Narration JAMBO FM

CCM SINGIDA MJINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI MANISP...

0:00 --:--

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Manispaa ya Singida, ikieleza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa kwa vitendo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Bi. Lucia Mwiru, amesema hayo wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati hiyo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Manispaa ya Singida.

Amesema Manispaa hiyo imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa Ilani ya CCM, hususan katika sekta za elimu na afya, pamoja na uwezeshaji wa vikundi vya uzalishaji kupitia mikopo ya asilimia 10.

Katika ziara hiyo, Kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi Mwachichi iliyopo Kata ya Mwankoko, Shule Mpya ya Msingi Unyamikumbi B katika Kata ya Kisaki, Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Mungumaji, pamoja na kikundi cha Fighters cha Madereva Bajaji kilichopo Kata ya Misuna na ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Kindai.

Aidha, Kamati hiyo imeipongeza Manispaa ya Singida kwa kuwaondoa wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kwa hiari, huku Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, akiipongeza Manispaa kwa ushirikiano mzuri na taasisi za Chama na kuahidi kuendelea kuisimamia ili miradi yote ikamilike kwa wakati.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.