Skip to main content

CCM MBULU WATAKIWA KUWA MABALOZI WA KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbulu wametakiwa kuwa mabalozi wa kutangaza mafanikio ya Serikali na Chama kwa kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.

CCM MBULU WATAKIWA KUWA MABALOZI WA KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbulu wametakiwa kuwa mabalozi wa kutangaza mafanikio ya Serikali na Chama kwa kueleza kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbulu, Ndg. Melkiad Naari, wakati wa mkutano wa kusoma na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026, uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za CCM Wilaya ya Mbulu.

Akizungumza katika mkutano huo, Ndg. Naari amesema kila mwanachama wa CCM ana wajibu wa kuwa msemaji wa mafanikio ya Serikali kwa kuwafahamisha wananchi hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo sekta za elimu, afya, maji, miundombinu na huduma nyingine za kijamii.

Amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na uongozi madhubuti wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo yanapaswa kufahamishwa kwa wananchi kwa usahihi ili waweze kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali yao.

“Niwaombe ndugu wajumbe, Serikali ya CCM inaendelea kufanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo katika Wilaya yetu. Chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kuwanufaisha wananchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu mafanikio haya na namna Chama kinavyotekeleza ahadi zake kupitia Ilani,” amesema Ndg. Naari.

Aidha, Mwenyekiti huyo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu kwa usimamizi na uratibu mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na miradi ya maendeleo, akieleza kuwa utendaji wake umechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya hiyo.

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa Chama, Serikali na wananchi ni msingi muhimu wa kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kuendelea kuwaletea wananchi huduma bora.

Mkutano huo ulikuwa sehemu ya utaratibu wa Chama wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kujadili mafanikio yaliyopatikana pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa malengo yaliyobaki kwa kipindi kinachofuata.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.