Skip to main content

CCM KIGOMA YATAKA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MIRADI

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma wameeleza kutoridhishwa na utendaji kazi na usimamizi wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za mkoa huo.

CCM KIGOMA YATAKA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MIRADI
Studio Narration JAMBO FM

CCM KIGOMA YATAKA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MIRADI

0:00 --:--

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma wameeleza kutoridhishwa na utendaji kazi na usimamizi wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za mkoa huo.

Wajumbe hao waliibua hoja mbalimbali, ikiwemo baadhi ya wakandarasi kuondoka katika maeneo ya miradi na kutokomea kusikojulikana kabla ya kukamilisha kazi walizopewa, huku baadhi ya miradi ikitelekezwa bila kukamilika.

Hoja hizo ziliibuliwa katika kikao cha Kamati ya CCM Mkoa wa Kigoma kilicholenga kutoa tathmini na majumuisho ya ziara iliyofanywa na kamati hiyo ya kutembelea na kukagua miradi 35 ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya mkoa.

Baadhi ya wajumbe wa CCM Mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye kikao, Picha na Tryphone Odace

Wajumbe walisisitiza kuwa kuna umuhimu wa watendaji wa serikali kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati, inakuwa na ubora unaotakiwa na thamani ya mradi iendane na fedha zilizotolewa.

Kwa mujibu wa wajumbe hao, usimamizi madhubuti wa miradi utasaidia kuongeza thamani ya fedha za umma na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Jamal Tamimu, amesema Serikali imeendelea kupeleka fedha nyingi mkoani humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwemo afya na elimu.

Alisema changamoto kubwa inayojitokeza ni namna fedha hizo zinavyosimamiwa na kutumika katika utekelezaji wa miradi, akisisitiza kuwa usimamizi usioridhisha unaweza kusababisha wananchi kuilalamikia Serikali hata pale ambapo fedha zimetolewa kwa ajili ya miradi hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma mwenye kofia akiwa kwenye picha na baadhi ya wajumbe, Picha na Tryphone Odace

Tamimu amewataka watendaji kuwajibika katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi na kuhakikisha wananchi wanapata miradi yenye ubora na inayokidhi mahitaji yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ambaye katika kikao hicho alikuwa Kamisaa, alisema Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa vitendo katika Mkoa wa Kigoma.

Balozi Sirro amesema utekelezaji wa miradi hiyo umeendelea kutoa mchango katika kuboresha maisha na kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, Picha na Tryphone Odace

Alitaja baadhi ya sekta zinazonufaika na uwekezaji huo kuwa ni elimu, kilimo, mifugo, afya, umeme na ujenzi wa barabara.

Aidha alisisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia miradi hiyo ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika ipasavyo na wananchi wanapata huduma zinazokusudiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.