Shirikisho la Soka Barani afrika (CAF), imebatilisha matokeo ya fainali ya AFCON na kuwapa ubingwa wa mezani Morocco ya ushindi wa 3–0.
CAF, kupitia bodi yake ya rufaa imetoa uamuzi kuwa Senegal ilipoteza fainali hiyo baada ya timu yake kuondoka uwanjani kulalamikia penalti waliyopewa Morocco.
Sheria za CAF zinasema kama timu inakataa kucheza au kuondoka uwanjani basi inaondolewa mashindanoni.

Senegal iliifunga Morocco 1–0 katika fainali ya Januari 18 iliyogubikwa na tukio ambalo wachezaji wa Senegal waligoma kucheza baada ya wenyeji kupewa penalty ya dakika za majeruhi.
Mechi hiyo ilisimama kwa dakika 17 na baadaye wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani na penalti iliyopigwa na Brahim Diaz ikaokolewa na kipa kabla ya Pape Gueye kufunga bao la ushindi katika muda wa ziada. #dwkiswahili
Discussion
Reader comments
0 contributions