Skip to main content

BUTIAMA YAWEKA MIKAKATI KUIMARISHA USIMAMIZI MIKOPO YA ASILIMIA 10

Na Adam Msafiri - Mara.

BUTIAMA YAWEKA MIKAKATI KUIMARISHA USIMAMIZI MIKOPO YA ASILIMIA 10

Na Adam Msafiri - Mara.

Halmashauri ya wilaya ya Butiama mkoani Mara, imeanza kuchukua hatua za kuimarisha usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 baada ya kubainika baadhi ya vikundi vilivyonunua pikipiki zilizotumika kwa fedha za mikopo,hali inayoweza kuhatarisha urejeshaji wa fedha na kuibua hoja za ukaguzi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Butiama George Machela amesema, Halmashauri hiyo haitavumilia matumizi yasiyoendana na malengo ya mikopo,ambayo imenzishwa na serikali kuwawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi.

Amesema baada ya kubaini baadhi ya vikundi vilinunua pikipiki zilizotumika bila utaratibu unaohitajika, Afisa maendeleo ya jamii ameagizwa kuzishikilia pikipiki hizo kwa muda ili zikamilishiwe usajili na nyaraka muhimu zitakazosaidia kulinda mali za vikundi pamoja na kuondoa hoja zinazoweza kujitikeza katika ukaguzi wa hesabu za serikali.

Mbunge wa Jimbo la Butiama Dkt Wilson Mahera amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.