Skip to main content

BUNGE GRAND BONANZA: PAMOJA AFCON 2027 NI ISHARA YA UTAYARI WA TANZANIA - SILLO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

BUNGE GRAND BONANZA: PAMOJA AFCON 2027 NI ISHARA YA UTAYARI WA TANZANIA - SILLO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema Bunge Grand Bonanza la mwaka huu lililobeba kaulimbiu ya “Pamoja AFCON 2027” ni ishara ya utayari wa Tanzania kuelekea maandalizi ya michuano hiyo pamoja na kuendeleza umoja na mshikamano wa kitaifa kupitia michezo.

Sillo ameyasema hayo leo Juni 20, 2026 wakati akiongoza bonanza hilo lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, likiwa na lengo la kuimarisha mshikamano, afya na ushirikiano wa kidiplomasia kupitia michezo.

"Tukio hili ni muhimu kwa maslahi mapana ya taifa letu katika kuimarisha umoja na ushirikiano miongoni mwetu na mataifa mengine kupitia michezo, Grand Bonanza la mwaka huu ni sehemu ya kuujulisha ulimwengu kuhusu utayari wa Tanzania katika kuandaa michuano ya michezo ya AFCON 2027,"amesema. 

‎Bonanza hilo limewakutanisha Wabunge, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini pamoja na wadau wa michezo, ambao wameonesha umoja na ushirikiano katika shughuli mbalimbali zilizoratibiwa kwa ajili ya tukio hilo.

‎Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema AFCON 2027 si mashindano pekee bali ni fursa muhimu ya kiuchumi na jukwaa la kuitangaza Tanzania kimataifa.

Naye, Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Festo Sanga amesema kupitia bonanza hilo imedhilisha kuwa Tanzania ipo tayari kwaajili ya michuano ya ya AFCON 2027.

‎Katika bonanza hilo washiriki wamepata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio fupi, pete, bao na kuvuta kamba, huku michezo hiyo ikitawaliwa na ushindani wa kirafiki na burudani.

‎Aidha, limekuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali kujadili namna ya kuunga mkono jitihada zinazoendelea kuhakikisha Tanzania inajiandaa kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya mashindano ya kimataifa.

‎

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.