Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema Serikali inapaswa kuongeza nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kwa kupunguza matumizi ya magari yanayotumia mafuta kwa kiwango kikubwa kama V8, ili fedha zaidi zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.
Bulaya ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia Bajeti ya Serikali hii leo Juni 16, 2026 na kuongeza kuwa, bajeti inayotarajiwa kupitishwa ina kiwango kikubwa cha kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 74, jambo linalohitaji umakini katika ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi.

Amesema, "Tanzania inapaswa kujiandaa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazoweza kujitokeza kadri Nchi inavyoendelea kujitegemea zaidi kifedha, huku akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali."
Discussion
Reader comments
0 contributions