Skip to main content

BOTI MPYA YA DORIA KUSAIDIA KUONGEZA MAPATO YA UVUVI BUKOBA

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

BOTI MPYA YA DORIA KUSAIDIA KUONGEZA MAPATO YA UVUVI BUKOBA

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba imenunua boti mpya ya kisasa ya doria yenye thamani ya Shilingi 42,291,202.36 ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi na kuongeza ukusanyaji wa mapato yatokanayo na sekta hiyo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mwenendo wa kupungua kwa mapato ya ushuru wa uvuvi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, hali iliyochangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na baadhi ya wavuvi kufanya shughuli zao nje ya utaratibu rasmi na hivyo kukwepa kulipa tozo na ada zinazotakiwa kisheria.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya manispaa ya Bukoba Bwana Jacob Nkwera alieleza kuwa chombo hicho kitasaidia kuongeza ufanisi wa doria katika maeneo ya uvuvi ndani ya Ziwa Victoria, kubaini na kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu pamoja na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za sekta ya uvuvi zinazingatiwa na wadau wote.

Aidha, uwepo wa boti hiyo unatarajiwa kuimarisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi, kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wanaotegemea shughuli za uvuvi kama chanzo cha kipato.

Bwana Nkwera alieleza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma na kuhakikisha sekta ya uvuvi inaendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya Manispaa ya Bukoba na ustawi wa wananchi wake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.