Skip to main content

BODABODA MWARUFYO MFANO WA KUIGWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI SINGIDA

Kikundi cha bodaboda cha Kijiji cha Mwarufyo, Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida, kimekuwa mfano wa kuigwa kwa kuunganisha nguvu zao katika miradi ya kiuchumi inayowawezesha kujikwamua kupitia ufugaji, kilimo na biashara.

BODABODA MWARUFYO MFANO WA KUIGWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

BODABODA MWARUFYO MFANO WA KUIGWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI SINGI...

0:00 --:--

Kikundi cha bodaboda cha Kijiji cha Mwarufyo, Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida, kimekuwa mfano wa kuigwa kwa kuunganisha nguvu zao katika miradi ya kiuchumi inayowawezesha kujikwamua kupitia ufugaji, kilimo na biashara.

Katibu wa kikundi hicho, Jeremia Ng'aida amesema kikundi chenye wanachama 35 kwa sasa kinamiliki ng'ombe watano wa kisasa wa maziwa na shamba la hekta moja linalolimwa mahindi, maharagwe na vitunguu. Miradi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 16 imeanzishwa kwa michango ya wanachama wenyewe bila kutegemea mikopo, ambapo kila mwanachama huchangia shilingi 2,000 kila wiki.

Jeremiah Nga'aida Katibu wa Kikundi cha Maafisa Usafirishaji Kijiji cha Mwarufyo Singida Dc

Amesema kwa sasa ufugaji huo unawawezesha kupata lita 12 za maziwa kwa siku, huku kikundi kikiendelea na ujenzi wa fremu tano za maduka kwa lengo la kuongeza vyanzo vya mapato na kukuza mtaji wao.

Mradi wa Ng'ombe wa Maziwa unaomilikiwa na Kikundi cha Maafisa Usafirishaji Kijiji cha Mwarufyo Singida Dc.

Pamoja na mafanikio hayo, kikundi kimeomba Serikali kutoa elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kupitia Halmashauri ili waweze kuomba mkopo wa kununua guta na zana za kilimo. Pia kimeomba kuungwa mkono ili kukamilisha ujenzi wa fremu hizo ambao umefikia hatua ya lenta.

Mradi wa Shamba unaomilikiwa na Kikundi cha Maafisa Usafirishaji Kijiji cha Mwarufyo Singida Dc.

Wanakikundi cha Maafisa Usafirishaji Kijiji cha Mwarufyo Singida Dc

Kikundi hicho kimetembelewa na Rais wa BODABODA CHAMAPITA Taifa, Michael Haule akiambatana na Mwenyekiti wa CHAMAPITA Mkoa wa Singida, Abdul Mitigo, baada ya kupata taarifa za mafanikio yake. Katika ziara hiyo, Haule aliahidi kukiunga mkono kikundi hicho kupitia CHAMAPITA Taifa.Rais wa Pikipiki na Bajaji Taifa CHAMAPITA, Michael Haule.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.