Skip to main content

BIMA YA AFYA KWA WOTE: DODOMA YATAKA KILA KIONGOZI KUWA SEHEMU YA UTEKELEZAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka viongozi wa Halmashauri kuwa na mipango ya utekelezaji inayoainisha idadi ya wananchi wanaolengwa katika mpango wa Bima ya afya kwa wote katika maeneo yao, mikakati ya utoaji elimu na namna ya kufuatilia utekelezaji wake.

BIMA YA AFYA KWA WOTE: DODOMA YATAKA KILA KIONGOZI KUWA SEHEMU YA UTEKELEZAJI
Studio Narration JAMBO FM

BIMA YA AFYA KWA WOTE: DODOMA YATAKA KILA KIONGOZI KUWA SEHE...

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka viongozi wa Halmashauri kuwa na mipango ya utekelezaji inayoainisha idadi ya wananchi wanaolengwa katika mpango wa Bima ya afya kwa wote katika maeneo yao, mikakati ya utoaji elimu na namna ya kufuatilia utekelezaji wake.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 22,2026 na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa wakati wa uzinduzi wa Bima ya afya kwa wote awamu ya pili.

Shekimweri amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha suala la Bima ya Afya kwa wote halibaki kuwa jukumu la wataalamu wa afya au waratibu wa bima pekee, bali linakuwa sehemu ya majukumu ya viongozi katika ngazi mbalimbali.

"Afya ya wananchi ni msingi wa maendeleo, hivyo kila kiongozi anapaswa kujiuliza iwapo wananchi katika eneo analoliongoza wanafahamu mpango huo, namna ya kujiunga na huduma wanazostahili kupata,"amesema.

Aidha, ameongeza kuwa elimu kuhusu Bima ya aafya kwa wote inapaswa kushushwa moja kwa moja kwa wananchi katika maeneo wanayoishi na kufanya shughuli zao, badala ya kusubiri wafike katika ofisi za Serikali ndipo wapate uelewa kuhusu mpango huo.

"Mafanikio ya mpango huu hayatapimwa kwa idadi ya mikutano, hotuba au mabango yanayowekwa, bali kwa uwezo wa kuwafikia wananchi, kuwapa taarifa sahihi na kuhakikisha wanaweza kupata huduma wanapozihitaji,"amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma Irene Kataraihya amesema mpango huo hautoishia kwenye Zahanati au kituo cha afya kwa utaratibu wa rufaa mwananchi ataweza kufika mpaka hospitali ya Mkoa.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote inaanzia kwenye uelewa wa mwananchi, kabla ya kufikia lengo la kuongeza idadi ya wananchi wanaojiunga na kutumia huduma za afya kwa mujibu wa mpango huo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.